This archive report was first published on 15 November 2019.
Maafisa wa polisi kaunti ya Siaya wanaendelea kuchunguza kifo cha mtahiniwa wa KCSE mmoja aliyefariki baada ya kufanya mtihani wake wa somo la biolojia.
Alama huyo alikuwa Fredrick Juma, mwanafunzi wa shule ya upili ya Memba eneo bunge la Rarieda, ambaye alianza kuugua Ijumaa, Novemba 15, dakika chache kabla ya kuaga dunia.
Mkurugenzi mkuu wa Elimu kaunti ya Siaya, Joseph Wamocho, alibainisha kuwa Juma alizarai na alipokimbizwa katika hospitali ya St. Mary's Lwak, aliaga dunia kabla ya kuhudumiwa na madaktari.
Hii ni kisa la pili kwa siku moja baada ya kifo cha mtahiniwa mwingine wa KCSE ambaye alifariki baada ya kufanya mtihani wake wa somo la Kemia katika kaunti ya Nakuru.