Skip to main content

Seneta Murkomen Amtishia Rais Uhuru Kenyatta Kuhusu BBI

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 15 November 2019.

Seneta Murkomen Amtishia Rais Uhuru Kenyatta Kuhusu BBI

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amemtishia Rais Uhuru Kenyatta kuhusu mswada wa BBI, akisema hatapendekeza chochote hadi Raila Odinga aombe msamaha kuhusu vurugu wakati wa uchaguzi mdogo wa Kibra.

Alisema hili wakati wa harambee ya kanisa la St Patrick eneo la Eldmana Ravin kaunti ya Baringo mnamo Jumapili, Novemba 10, 2019.

"Tunataka kusisitiza kwamba sisi kama viongozi wa Jubilee, hatutaunga mkono mswada wa BBI hadi pale ambapo Raila Odinga ataomba msamaha kuhusu machufuko ya uchaguzi na kukiri dhambi zake," alisema.

Aliongeza kuwa chama cha Jubilee hakitalipiza kisasi hata baada ya kupigwa mawe, lakini wanasiasa hao watakubali kuwa mtindo wa uongozi wa Raila ni wa fujo.

Alisema ni sharti kinara wa ODM Raila Odinga aombe msamaha kwanza hadharani kutokana na vurugu iliyoshuhudiwa hivi karibuni wakati wa uchaguzi mdogo wa Kibra.

Uchaguzi huo ulikumbwa na vurumai kati ya baadhi ya viongozi wa Jubilee na wakazi wa eneo hilo.

Seneta huyo alikuwa akizunguzia uchaguzi mdogo wa Kibra uliofanyika Alhamisi, Novemba 7, ambapo mbunge wa Kimilili Didmus Barasa na aliyeo kufuata seneta wa Kakamega Boni Khalwale walivamiwa na wakazi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →