Skip to main content

Mstaafu Daniel Moi Akimbizwa Tena Hospitalini

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 11 November 2019.

Alhamisi, Novemba 7, 2019, familia ya Mstaafu Daniel Moi ilimruhusu kwenda nyumani baada ya kulala katika hospitali hiyo wiki mbili.

Madaktari wake walimruhusu kwenda nyumani ingawa kufikia sasa, ugonjwa anaougua bado haujatajwa.

Alipolazwa tena Nairobi Hospital, Msemaji wa Mzee Moi Lee Njiru alisema kuwa, Moi alipelekwa hospitalini Jumamosi, Novemba 9 kufanyiwa "uchunguzi wa kawaida”.

Lee Njiru aliongeza kuwa, Moi yupo macho, anafahamu kinachoendelea na anahudumiwa na mahudumu nguli wakiongzwa na daktari binafisi Dkt David Silverstein.

“Amelazwa eneo la watu mashuhuri VIP, eneo lenye mazingira kama ya nyumbani, kuruhusu uangalizi wa kila mara na matibabu yanayohitajika. Nawaomba wanahabari wasisambaze habari za kutia hofu,” Njiru alisema.

Awali familia ilikana madai yaliyokuwa yakisemaa kuwa, hali yake ilikuwa mbaya. Ilisema alikuwa timamu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →