This archive report was first published on 25 October 2019.
Mpelelezi wa binafsi Jane Mugo alichapisha picha yake akiwa na mwanawe wa kiume ambaye ni mtahiniwa wa mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne mwaka huu.
Mugo alichapisha picha hii kwa ajili ya kusherehekea mwanawe kwa kufaulu katika mtihani wa KCSE ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mugo aliandika, "Nina uhakika umejiandaa vema kwa miaka minne, najua utafaulu katika mtihani wako na utangaa zaidi kwani wewe ni nyota ya mama, kila la heri mwanangu."
Mugo pia aliwatakia heri njema watahiniwa wote wa mitihani ya kitaifa mwaka huu.
Habari hii inatokana na tarehe 25 Oktoba 2019.