Skip to main content

Mshukiwa Mkuu wa Mauaji ya Padri wa Machakos Alikuwa Mpenzi Wake, Makachero Wasema

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 24 October 2019.

Mshukiwa Mkuu wa Mauaji ya Padri wa Machakos Alikuwa Mpenzi Wake, Makachero Wasema

Uchunguzi uliofanywa kwa mauaji ya padri wa Machakos Michael Kyengo ulionyesha kuwa mshukiwa mkuu wa mauaji hayo alikuwa mpenzi wake.

Michael Muthini, mwalimu wa shule ya msingi, alikamatwa na maafisa wa polisi akiwa na gari la marehemu na aliandamana nao hadi eneo alikozikwa mwenda zake karibu na mto.

Aliongeza kuwa mshukiwa alimtumia kuhani huyo ujumbe wa "hi dear" naye akamjibu "hi my love".

Uchunguzi wa mnamo Oktoba 7 ulionesha kuwa wawili hao walikuwa wakitumiana jumbe na kuitana majina wanayotumia wachumba.

Maafisa wa polisi walipigwa na butwa baada ya mshukiwa kukiri kwamba alikuwa mchumba wa kuhani huyo na alianza kuingiwa na wasiwasi akihisi huenda alikuwa ameanza kumpuuza.

Julio Mutembei, afisa anayehusika na uchunguzi huo, aliiomba mahakama kumpa siku 14 zaidi kukamilisha uchunguzi kabla ya kesi ya mshukiwa kuanza rasmi.

Alipewa muda wa siku 10 na hakimu Hellen Okwami kukamilisha uchunguzi wake.

Muthini alikamatwa mnamo Alhamisi, Oktoba 15, na maafisa wa kitengo maalum cha kupambana na uhalifu akiwa na gari aina ya Toyota Axio KCQ 665S linalomilikiwa na padri huyo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →