Skip to main content

Wanafunzi walioketi maboxi kufanya mtihani wa kemia kwa ajili ya kuzuia wizi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 21 October 2019.

Shule moja nchini India ilikuwa na suala la kujisikia baada ya picha za wanafunzi waliopigwa picha wakifanya mtihani wa kemia wakiwa wamevalia maboxi vichwani kusambaa.

Wanafunzi hao walikuwa wakifanya mtihani wa somo la kemia wakati picha hizo zilipigwa wakati wa tarehe 21 Oktoba 2019.

Maafisa wa elimu eneo hilo walijitokeza kwa haraka kulalamikia suala hilo baada ya picha hizo kusambaa.

"Nilipopata ujumbe kuhusu haya, nilienda kwa shule hiyo haraka na kuamuru usimamizi wa shule hiyo kusitisha mpango huo. Pia nilitoa notisi kwa usimamizi wa shule hiyo na ninapania kuwachukulia hatua ya kinidhamu dhidi yao," alisema SC Peerjade, ambaye ni naibu mkurugenzi wa elimu ya vyuo vikuu.

Shule hiyo iliomba radhi kwa umma huku ikisema mpango huo ulitekelezwa ili kuzuia udanganyifu wa mtihani lakini imesitishwa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →