Skip to main content

Wazito FC wanaripotiwa kuwafuta kazi maafisa wao wote wa ushahuri

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 20 October 2019.

Wazito FC, klabu ya Ligi Kuu ya Kenya, imepewa kichapo cha msimu mpya baada ya kushindwa kwa kikosi chake kwa Kakamega Homeboyz. Kichapo hicho kilikuwa kwa sababu ya matokeo mabovu waliondikisha kuanzia msimu mpya.

Imebainika kuwa kocha Fred Ambani, mwenzake Hamisi Abdalla na Mkurugenzi Mkuu wa Ushahuri Stanley Okumbi wameagizwa kupanga virago.

“Hongera Kakamega Homeboyz kwa ushindi wenyu. Walifaa kupata ushindi huo huku safu yetu ya ulinzi wakionekana kana kwamba walitokea KFC. Ninaomba radhi mashabiki wetu na ninaahidi kufanya marekebisho yanayoitajika,” aliandika Ricardo Badoer, mmiliki wa klabu, kwenye Twitter.

Wazito FC ilipandishwa daraja hivi majuzi na sasa imeishikilia nafasi ya 13 kwenye jedwali kati ya timu 18 zilizooredheshwa.

Imebainika kuwa kumekuwa na uhasama kati ya Ambani na Okumbi, ambao wote ni makocha wa timu ya taifa ya wachezaji walio chini ya miaka 20 na pia awali walinoa timu ya Harambee Stars.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →