This archive report was first published on 9 October 2019.
Maafisa wa polisi wamezingira nyumba ya Bobi Wine, mbunge wa Uganda, ili kumzuia kuhudhuria hafla ya muziki kuhusu siku ya uhuru nchini humo.
Bob Wine alionyesha picha za maafisa wa polisi pamoja na wanajeshi aliosema kuwa wamezingira nyumba yake.
Aliongeza kuwa nia yao ni kuhakikisha hajafika kwenye hafla hiyo na hivyo kukosa kuikosoa serikali.
Alisema kupitia mtandao wake wa twitter, Jumatano, Oktoba 9, kuwa maafisa wa polisi wamezingira nyumba yake eneo la One love beach Busabala.
Alisema kuwa nia yao ni kumzuia kuhudhuria hafla ya muziki kuhusu uhuru wa nchi ili nisikosoe serikali.
Alisema kuwa sasa siwezi kuimba katika nchi yangu.
Bob Wine amejijengea jina kwa kuwa mkosoaji mkuu wa Rais Museveni katika kipindi ambapo wengi bado wanamhofia.