Skip to main content

Ben Githae aongoza wasanii kumsifu Uhuru, mashabiki wakataa wito wake

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 29 June 2020.

Ben Githae, msanii wa nyimbo za injili, amekashifiwa vikali kwa kuimba wimbo wa kusifia Rais Uhuru Kenyatta na kuwakashifu wanaokosoa uongozi wake.

Wimbo huo ulikuwa na waimbaji wengine kutoka Mlima Kenya, ambao walimshabikia Rais kutoa upanga wake ili kuwaangamiza wote ambao wanampinga.

Walisema wanaoenda kinyume na Rais ni kama mwana Absalom kwenye Biblia, ambaye alipewa utajiri na babake lakini akamgeuka na kuanza kuwachochea wanaIsraeli.

Walisema Rais anafaa kutoa upanga wake kama mfalme na awatenganishe wafuasi wake na wale wasiomfuata.

Video iliyotolewa inaonyesha wapinzani wa Rais, kama vile Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria, wa Kapseret Oscar Sudi, Ndindi Nyoro, na Rigathi Gachagua.

Walikosa kuamini wimbo huo na badala yake wakamuingia Githae pamoja na wenzake.

Wanamtandao walihisi wimbo huo ni wa kumpaka kiongozi wa taifa mafuta bure huku hali ikiwa tofauti mashinani.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →