This archive report was first published on 28 December 2019.
Si lazima DP Ruto awe rais 2022, Raila asema ¶
Kinara wa ODM Raila Odinga amesema 2022 si William Ruto pekee anataka kuwa rais. Picha: State House
Alisema ni Wakenya wengi sana wanataka kuwa rais na hivyo haifai kuwa na mjadala kana kwamba ni Ruto pekee atakuwa akiwania kiti hicho.
Alisema hii kwa mara ya kwanza kwenye mahojiano na runinga ya Citizen Ijumaa, Disemba 27.
Alisema handisheki yake na Rais Uhuru Kenyatta sio kuhusu kugombea wadhifa wowote wa kisiasa mbali kutataua shida zinazowakumba Wakenya.
Alisema BBI ni muhimu kwani ilizaliwa baada ya mkutano wenye kijibaridi kati yake na Rais Uhuru Kenyatta.
Alisema mkutano huo ulikuwa na wao wawili tu na hata Rais alijileta kwa gari na akachelewa baada ya kukwama kwenye msongamano wa magari.
Alisema wawili hao walifika kwenye kikao hicho kama washindani sawa ili kujadili tatizo lililokuwepo.
Alisema hata Rais Kenyatta, licha ya kuwa mmoja wa watu ambao hupewa ulinzi mkali nchini, aliwahepa maafisa wake wa usalama na kuelekea kwenye mkutano huo.
Alisema tulijipeleka kwenye kikao hicho, Rais alijileta mwenyewe kwa gari na mimi pia nilijileta kwa gari. Rais alikwama kwenye msongamano wa magari na kuchelewa, ulikuwa ni mkutano wetu tu wawili.