This archive report was first published on 27 December 2019.
DP Ruto: Naweza Jitoa Kwa Siasa Za 2022 ¶
Naibu Rais William Ruto amesema hataki Wakenya kupigana kwa sababu ya ndoto yake ya kuwa rais.
Alisema hivyo wakati wa mkutano na wazee wa jamii ya Agikuyu wakiongozwa na mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri uliofanyika nyumbani kwake Sugoi, Disemba 19.
DP Ruto alisema hataki Wakenya wauane kwa sababu ya siasa, na kuwaambia kundi hilo la wafuasi kwamba ushirikiano wake na Rais Uhuru Kenyatta kabla ya uchaguzi wa 2013 haukuwa wa kushinda urais tu.
Alisema, "Hatukuungana na Uhuru Kenyatta kushinda uchaguzi. Tuliungana ili kumaliza ukabila na chuki, kushinda uchaguzi ni nyongeza tu, hakuna kiongozi ambaye hajachaguliwa na Mungu."
DP Ruto alisema waliungana na Uhuru Kenyatta ili kumaliza siasa za chuki na ukabila humu nchini. Picha: William Ruto
Alisema hivyo wakati wa mkutano na wazee wa jamii ya Agikuyu wakiongozwa na mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri uliofanyika nyumbani kwake Sugoi, Disemba 19.
DP Ruto alisema hataki Wakenya wauane kwa sababu ya siasa. Picha: William Ruto
Alisema, "Afadhali nijiondoe kwenye mbio za urais kuliko Wakenya wauane kwa sababu ya siasa."
DP Ruto alisema hataki Wakenya kupoteza maisha yao kwa sababu ya kumuunga mkono kisiasa. Picha: UGC
Alisema hivyo wakati wa mkutano na wazee wa jamii ya Agikuyu wakiongozwa na mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri uliofanyika nyumbani kwake Sugoi, Disemba 19.
Alisema, "Sitaki Wakenya kupigana kwa sababu yangu. Na hilo ni kuhimu sana kwangu. Sitaki Mkenya yeyote kupoteza maisha kwa sababu ya mwanasiasa fulani. Nishindi ama nisishinde, amani ndio muhimu zaidi."
DP Ruto alisema hataki Wakenya wauane kwa sababu ya siasa. Picha: William Ruto