Skip to main content

Wakazi wa Kisumu waachwa bila makao baada ya mafuriko kuharibu nyumba zao ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 27 December 2019.

Wakazi wa Kisumu waachwa bila makao baada ya mafuriko kuharibu nyumba zao ▷ Kenya News

Wakazi wa Kisumu wametoa wito kwa serikali ya kitaifa na ile ya kaunti kushughulikia suala la mafuriko ambalo limekuwa kero kwao.

Mvua kubwa ilianza kunyesha Jumatano, Disemba 25, na kuendelea kwa zaidi ya saa tano huku maji yakifurika katika nyumba za wakazi na kwenye barabara.

Mvua hiyo ilisababisha hasara kubwa katika eneo la Nyamasaria na viungani mwa Kisumu.

Mto wa Nyamasaria vile vile ulivunja kingo zake na kusababisha mafuriko zaidi katika sehemu zilizoko karibu na eneo hilo.

Wakazi wa Kisumu walazimika kuhamia sehemu zilizoinuka baada ya nyumba zao kufurika maji.

Mmoja wa wakazi hao alilalamika, "Tunaiomba serikali ya kutaifa, ile ya kaunti na wahisani kutusaidia na bidhaa za matumizi nyumbani. Mali yetu yote imeharibiwa na maji. Hatuna chakula. Siku saba sasa hatujaona hatua yoyote ikichukuliwa kutoka kwa serikali,".

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →