This archive report was first published on 26 December 2019.
Wanaume Wanapenda Wanawake Wenye Makalio Makubwa, Utafiti Waonyesha ¶
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu Bilkent, Chuo Kikuu cha Texas, na Chuo Kikuu cha American University kilichoko jijini Beirut ulibaini kuwa wanaume wengi wanapenda wanawake waliojaaliwa makalio makubwa.
Imebainika kuwa, kinachowavutia wanaume sio makalio hasa bali ni kupinda kwa uti wa mgongo unaosababisha kalio kuwa kubwa zaidi.
Wakati wa utafiti huo, wanaume walioneshwa picha za makalio ya wanawake wengi na asilimia kubwa iliwapendelea wanawake waliokuwa na uti wa mgogo uliopinda kwa kiwango cha 45.5.
Asilimia 30 ya waliooa kila mmoja alisema ikiwa angepewa nafasi ya kuchagua tena, basi angelimchukua mwanawake mwenye makalio makubwa zaidi kuliko yule aliye naye sasa.
Utafiti huo ulisema, katika miaka ya awali mwanamke aliyeonekana kuwa na makalio makubwa alipendelewa kutokana na uwezo wake wa kubeba mizigo mgongoni.
Isitoshe mwanamke wa aina hiyo aliwavutia wanaume wengi na hivyo alikuwa na uwezo wa kuzaa watoto wengi.
Imebainika kuwa, mwanamke aliyejaaliwa nyuma angeweza kustahimili uzito wa mtoto aliyebebwa tumboni na hata kutopatwa na makali ya mimba ikilinganishwa na wale wenye makalio wastani.