This archive report was first published on 26 December 2019.
Wakati wa kusherekea kuzaliwa kwa Kristo Disemba 25, 2019, katika kanisa la ACK Nyamira huko Bondo, Raila Odinga alisema kanisa linahitaji maombi ili kujikomboa na kuvua ngozi ya ufisadi.
Alisema hilo kwa kusema kwamba kanisa linafaa lijiombee kwanza ili kujiokoa kutoka kwa minyororo ya ufisadi.
Alisema viongozi wa kanisa watakuwa na hatia iwapo watendelea kushirikiana na wale ambao wanaleta pesa kanisani ambazo hazijulikani zimetoka wapi.
Alisema ingawa kanisa haifai kuegemea upande wowote kuhusiana na siasa, ina jukumu la kukemea wanasiasa waovu kwenye jamii.
Alisema DP Ruto amekuwa akishiriki michango kanisani ambapo hutoa mamilioni kila wiki, huku akipuuza wanaomkosoa na kusema yeye alifunzwa kumtolea Mwenyezi Mungu.
Alisema serikali inafanya juhudi kuhakikisha hali ya kiuchumi itaimarika kufikia mwaka wa 2020.