This archive report was first published on 25 December 2019.
Wavuvi 8 wamepatikana hai baharini baada ya mashua yao kuzama Disemba 8, 2019, katika eneo la Ziwayu, kaunti ya Kilifi, Kenya.
Wavuvi hao walipatikana Jumatano, Disemba 25, wakiwa katika hali mbaya na kukimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi.
Waliposhindwa kudhibiti mashua hiyo waliruka majini ili kujiokoa na wamekua wakitafuta njia ya kujitoa majini.
Wavuvi hao walikuwa kwenye mashua ya Alhafidh Fibre 15HP ambayo ilipigwa na mawimbi makali na hivyo kuzama.
Walikuwa wakivua samaki wakati mashua yao ilipigwa na mawimbi makali na kuzama Disemba 8, 2019.
Wavuvi hao walipatikana na kundi lingine la wavuvi na kuokolewa.