This archive report was first published on 25 December 2019.
Rais Uhuru Kenyatta na familia yake walikaribisha kuzaliwa kwa Kristo katika kanisa katoliki la St Francis of Assisi eneo bunge la Nyali, Mombasa, kwa ajili ya sherehe za krisimasi.
Aliwataka Wakenya kuishi kwa amani na kuendeleza ujenzi wa taifa, huku akiongea kwenye kania hilo.
Alitoa pongezi kwa kanisa kutokana na juhudi zake za kuwaunganisha Wakenya na pia kuunga mkono vita dhidi ya ufisadi.
Uhuru aliwataka Wakenya kuendelea kuishi pamoja kwa amani ili taifa lisonge mbele, huku akiongeza kwamba Wakenya waendelee kudumisha amani na kuisha kama ndugu ili Kenya iweze kupiga hatua za maendeleo.
Washirika wa kanisa hilo walipata nafasi ya jumuika na Rais pamoja na familia yake huku akiwa na ulinzi mdogo tu.
Uhuru alionekana na walinzi wachache tu ambao walikuwa wamevalia kama raia, tofauti na wakati wa shughuli za kiserikali.
Published on December 25, 2019.