Skip to main content

Wazazi Wafariki Kwenye Ajali Kwa Sikukuu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 24 December 2019.

Sherehe za Krisimasi zilikuwa zimekuwa na madhara makubwa kwa familia za watu wengi, kama vile ile ya mume na mke ambao waliuawa kwa ajali wakisafiri mashambani kwa sherehe za Krisimasi, 24 Dsiemba 2019.

Matatu waliyokuwa wakisafiria abiria hao ilipoteza mwelekeo kwenye daraja la Mwiwondwe barabara ya Ekero-Buyangu na kubingirika, na kusababisha ajali ambayo ilikuwa na madhara makubwa.

Madereva wametakiwa kuwa makini kipindi hiki ili kuzuia kilio kwa familia baada ya kuwapoteza wapendwa wao.

Matatu hiyo ilikuwa ikisafiri kuenda Busia na ajali hiyo imewaacha watu wengine watano wakiwa na majeraha mabaya.

Miili ya waliofariki ilipelekwa katika hifadhi ya maiti ya St. Marys Mumias Hospital.

Wasafiri kwenye barabara ya Mai Mahiu walikwama kwenye msongamano kwa masaa kadhaa baada ya wafugaji kufunga barabara hiyo wakilalamikia mifugo wao kugongwa.

Madereva wametakiwa kuwa makini barabarani wakati huu wa sherehe za Krisimasi ili kuepuka ajali zaidi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →