Skip to main content

Duale: DP Ruto's Presidential Ambition Unstoppable

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 23 December 2019.

Aden Duale, kiongozi wa wengi bungeni, amesema kuwa ndoto ya Naibu Rais William Ruto kumrithi Rais Uhuru Kenyatta haiwezi kutatizwa na yeyote.

Amesema hilo litafanyika hata kama BBI itabadilisha mfumo wa uongozi humu nchini.

Amesema wote wanaojaribu kuhujumu safari hiyo wanapoteza muda na mali yao kwani tayari meli ya DP imeng'oa nanga kuelekea Ikulu.

Amesema DP Ruto ataingia Ikulu 2022 liwe liwalo.

Amesema kinara wa ODM Raila Odinga anajaribu kutumia jopo la uwiano, BBI, kumhujumu Ruto kisiasa.

Amesema, "Tuko tayari kumuunga mkono Ruto kabisa, hata BBI ipendekeze mfumo wa uongozi wa bunge au wa urais,".

Amesema DP Ruto yuko tayari kuwania urais 2022 kupitia mfumo wowote wa uongozi.

Amesema mojawapo wa mikakati yao ni kuhakikisha serikali ya Jubilee inatimiza ahadi zake kwa Wakenya ili Ruto awe na wakati rahisi kuomba kura 2022.

Amesema, "Jubilee iko na ahadi na Wakenya ya kuinua sekta ya afya, elimu na kutengeneza nafasi za kazi kwa vijana. Haya ndio mambo tunataka kushughulikia kwa miaka miwili ijayo,".

Amesema atastaafu siasa baada ya DP kufanikiwa kuingia Ikulu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →