This archive report was first published on 22 December 2019.
Seneta Millicent Omanga alikuwa anamtakia dadake heri njema katika siku yake ya kuzaliwa, Disemba 21, 2019.
Alimiminia mdogo wake Anita Omanga maneno matamu, kwa kusema, "Dada, ulizaliwa wa kipekee, na wa maansa sana. Ninajivunia kuwa na dada kama wewe maishani mwangu. Happy Birthdei," kwenye Facebook.
Ujumbe huo ulikuwa na athari kubwa kwa wanachama wa Team Mafisi, ambao wamekuwa wakimiminika kwenye ukurasa wa Facebook wa Seneta Mteule Millicent Omanga.
Maoni mengi yalitoka kwa wanaume ambao walikuwa wanababaishwa na urembo wa kidosho huyo, na baadhi yao walikuwa wanaomba kupata nambari yake ya simu na wengine kutaka hata kujua kama yuko katika ndoa.