This archive report was first published on 22 December 2019.
Polisi wa Kirinyaga wanaendelea kuchunguza kisa ambapo karatasi za kufungia bangi zilipatikana kwenye duka la MCA wa wadi ya Kabare mjini Kutus.
Karatasi hizo zilikuwa na karatasi takriban 700,000 ambazo zinajulikana kama rizla mtaani.
Maafisa wa polisi wanaerekodi ripoti kutoka kwa MCA huyo kuhusu kisa hicho.
“Karatasi hizo za kufungia bangi zinajulikana kama rizla. MCA wa wadi ya Kabare Chomba Nyaga tayari ameandikisha ripoti,” alisema Anthony Mbogo, Mkuu wa polisi eneo hilo.
Polisi wanamsaka mteja aliyeweka mzigo huo ili kubaini ukweli wa kisa hicho.
Maafisa wa polisi wanaendelea kuchunguza kisa hicho ili kubaini ni kosa gani kilichotokea.