This archive report was first published on 21 December 2019.
Mtangazaji Shaffie Weru amepinga madai yaliyosambazwa mitandaoni kwamba alihusika kwenye ajali iliyotokea eneo la Northen Bypass.
Kwa mujibu wa picha zilizosambaa mitandaoni, Shaffie anaonekana amesimama kando ya mabaki ya gari la aina ya Mercedes G Wagon, lenye thamani ya mamilioni ya pesa.
Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Shaffie alichapisha ujumbe akiwataka mashabiki zake kuwa watulivu kwani alikuwa yuko salama salmini na wala hakuhusika kwenye ajali yoyote.
"Sijahusika kwa ajali yoyote jinsi inavyosemwa. Nilikuwa nimeenda kumsaidia mwathiriwa wa ajali ambaye ni rafiki yangu. Mkiziangalia kwa makini picha zinazosambazwa mitandoani mtaona jinsi ninavyojishughulisha kusaidia pale ninapoweza," Shaffie alisema.
Shaffie alidokeza kwamba rafiki yake huyo ambaye hakumtaja alikuwa akielekea Nairobi kuhudhuria mchezo wa gofu kabla ya gari hilo kugongwa na lori eneo lake la mbele.