This archive report was first published on 20 December 2019.
Familia ya Jaji Odek Hukabiliana na Wafanyikazi wake ¶
Jaji wa Mahakama ya Rufaa James Odek alipatikana amefariki nyumbani kwake mnamo Jumatatu, Disemba 16. Familia yake ilikabiliana na wafanyikazi wake baada ya kuvamia boma lake kupanga mazishi yake.
Upasuaji wa maiti yake uliopangwa kufanyika Alhamisi, Disemba 19 ulisitishwa hadi tarehe isiyojulikana. Hata hivyo, wafanyikazi hao hawakuwa na budi ila kuwaruhusu jamaa wa mwendazake kuingia na kuanza kupanga mazishi yake.
Wazee wa mtaa wa Rarieda walivamia boma lake na kuanza mipango ya mazishi yake. Sokomoko ilizuka katika boma la marehemu baada ya jamaa ake kuingia kwa lazima kuanza mipango ya mazishi yake.
Alhamisi, Disemba 19, mabishano makali yalizuka katika boma la marehemu la Rarieda baina ya wafanyikazi wa Odek na jamaa zake. Wafanyikazi hao hawakuwa na budi ila kuwaruhusu jamaa wa mwendazake kuingia na kuanza kupanga mazishi yake.
Mapema asubuhi ya Jumatatu, Disemba 16, Jaji Odek alipatikana amefariki nyumbani kwake katika boma lake la Kisumu. Boma lake lililoko kijiji cha Memba, eneo bunge la Rarieda kaunti ya Siaya.
James Odek alianza kuhudumu katika mahakama ya rufaa 2012 baada ya juhudi zake za kutuma ombi la kuwa Jaji katika Mahakama Kuu kukosa kufaulu.