This archive report was first published on 19 December 2019.
Msichana wa umri wa miaka 17 amekamatwa Marekani baada ya kuingia kwa kuruka ua katika uwanja wa ndege jijini California na kuiba ndege kabla ya kusababisha ajali.
Msichana huyo aliingia katika uwanja wa ndege wa Yosemite Fresno na kuiba ndege aina ya King Air 200 mnamo Jumatano, Disemba 18.
Polisi wa Uwanja wa Ndege wa Fresno walisema walipokea habari kutoka 911 kuhusu tukio hilo na kujibu 7.30am.
Video ya mitandaoni ilionyesha ndege hiyo ikitolewa maegesho ikazungushwa mara kadhaa na hatimaye kupiga dafrao ua wa uwanja huo.
Wakati polisi wanafika, walimpata msichana huyo ndani ya dungu la ndege hiyo na kichwani alikuwa na vifaa vya mawasiliano vya rubani kichwani.
Polisi walipokuwa wakijaribu kumkamata, msichana huyo alizua fujo na kujaribu kukataa kukamatwa na kutiwa pingu.
Alipelekwa katika korti ya watoto na kushtakiwa kwa kosa la kuiba ndege.