Skip to main content

Uganda: Wafuasi wa Bobi Wine Wamebuni Mbinu Mpya ya Kampeni Baada ya Benki Kuu Kukatwa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 19 December 2019.

Benki ya Uganda iliyoshangazwa na picha za pesa za Uganda zikiwa na maandishi ya kampeni za kisiasa, wafuasi wa Bobi Wine wamebuni mbinu mpya ya kampeni.

Wafuasi hawa wameanza kutumia matunda na mboga sokoni na hata mabango kwa ajili ya kuwasilisha jumbe zao na kuhamasisha wenzao kumpigia mwanaiji wao kura 2021.

Ujumbe wa @JimmyEriclevi ulisema, "Bobi Nine huenda asihitaji pesa kujitangaza 2021."

Wafuasi wa Rais Yoweri Museveni na Bobi Wine walikuwa wakiweka maandishi ya kisiasa katika noti nchini humo wakiwahamasisha wenzao kumpigia mwanaiji wao kura 2021.

Gavana wa Benki Kuu nchini humo, Emmanuel Mutebile alisema, "Pia ni kuharibu kwa fedha na wanaomiliki pesa zilizo na maandishi huenda wakapoteza kwa kuwa huenda zikakosa thamani," na "Umma unashauriwa kupokea pesa safi zisizokuwa na maandishi yasiyokuwa ya Benki Kuu."

Bobi Wine amekuwa akiimarisha umaarufu wake wa kisiasa kila kukicha na licha ya kuhangaishwa na serikali ya Museveni, amekuwa akitumia fursa hiyo vyema kujiimarisha kisiasa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →