Skip to main content

Rais Trump Avuliwa Madarakani na Bunge la Wawakilishi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 19 December 2019.

Rais Trump Avuliwa Madarakani

Donald Trump, rais wa Marekani, amevuliwa madarakani na Bunge la Wawakilishi la Marekani, kufanya ajiweke kama rais wa tatu kubanduliwa katika historia ya Marekani.

Uvuliwaji huu ulikuwa kwa kura 230 dhidi ya 197 katika kipengee cha kwanza cha uchunguzi cha kutumia vibaya mamlaka, ambacho kilipitishwa na wabunge wa Bunge la Wawakilishi.

Trump alikuwa anatuhumiwa kwa kushinikiza Ukraine kuzindua uchunguzi dhidi ya hasidi wake wa siasa na makamo wa rais wa zamani Joe Biden.

Spika wa Bunge la Wawakilishi, Nancy Pelosi, alisema Trump ndiye aliwachochea wanachama wa Democrats kuendeleza kutimuliwa kwake ofisini.

Trump hataondoka ofisini ghafla kwani anatazamiwa kufika mbele ya Seneti, ambapo thuluthi mbili ya walio wengi katika Seneti wanatazamiwa kumhoji kabla ya kuamua hatma yake.

Wakati huo huo, Trump anashikilia kuwa hana makosa ya kubanduliwa ofisini kama anavyotuhumiwa na Democrats.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →