Skip to main content

Magenge ya Kihalifu Mombasa: Uhalifu Uko Kwa Uangalifu

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 18 December 2019.

Mombasa, kivutio cha utalii, imekuwa mji wa shaka kwa sababu ya visa vya utovu wa usalama. Magenge mapya ya kihalifu yanaendelea kuchipuka, na watu 40 wamekuwa wameuawa na makundi haya ya kihalifu katika kipindi cha mwaka mmoja.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika linaeleza kuwa watu 40 wamekuwa wameuawa na makundi haya ya kihalifu katika kipindi cha mwaka mmoja, huku wahalifu 30 wakiuawa na kukamatwa kwenye makabiliano na maafisa wa polisi.

Polisi hapa Mombasa wanazidi kutoa wito kwa wazazi na wakaazi kwa ujumla kufanya kazi pamoja nao katika kutoa taarifa zitakazopelekea kuwakamata wahalifu hao.

Idara ya usalama kupitia kamanda wa Likoni Jane Munywoki inasema, ingawa changamoto za polisi zipo lakini juhudi zao za kuwasaka na kuwakamata wahalifu hazilali.

“Tunaendelea na mikakati ya kuyasaka mageni ya kihalifu hivyo tunawataka wazazi wawatunze watoto wao kwa sababu wengi wao wana umri mdogo sana, wa kati ya miaka kumi hadi kumi na mitatu,” akasema Munywoki.

Shirika lisilo la serikali la Haki Afrika linashikilia kuwa kulingana na utafiti wao watu 40 wameuawa mikononi mwa makundi haya ya kihalifu katika kipindi cha mwaka mmoja, huku wahalifu 30 wakiuawa na kukamatwa kwenye makabiliano na maafisa wa polisi.

Polisi nao yadaiwa kuzembea kazini na kula milungula hali inayochangia kuathirika kwa usalama.

Mathias Shipeta, afisa wa Kitengo cha dharura kwenye shirika lisilo la kiserikali la Haki Afrika, anaeleza kwamba magenge haya yalichipuka kama makundi ya kucheza mpira kabla ya kuingilia uhalifu katika maeneo ya kisauni.

“Wanasiasa wengine waliwatumia vijana hawa na kuwaahidi mambo ambayo hawakuyatekeleza na imechangia pakubwa sana vijana hao kujiunga na uhalifu,” akasema Shipeta.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →