This archive report was first published on 18 December 2019.
Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria alitania waandamani waliofanya maandamano kwenye eneo bunge lake Jumatano, Disemba 18, 2019.
Maandamano hayo yalikuwa kwa kushutumu Kuria kwa madai ya kukosa kumheshimu Rais Uhuru Kenyatta.
Waandamanaji katika eneo bunge la Gatundu Kusini wakiteta dhidi ya mbunge wao. Picha: Moses Kuria
Maandamano hayo yalikuwa kwa kushutumu Kuria kwa madai ya kukosa kumheshimu Rais Uhuru Kenyatta.
"Leo maadui wa maendeleo walikuwa wamepanga maandamano ya mamilioni ya watu dhidi yangu Gatundu," alisema mbunge huyo matata.
"Yalikuwa makubwa sana hivi kwanga wanahistoria wa siasa walikimbia huko kuandika vitambu," Kuria alitania.
Mbunge huyo alitaka Wakenya wamuombee akisema kuna maadui ambao wanamuandama.
Mbunge huyo amekuwa mmoja wa wale ambao hukosoa uongozi wa Rais Uhuru Kenyatta hadharani huku akisema amesahau na wafuasi wake wa Mlima Kenya.