This archive report was first published on 18 December 2019.
Arteta, mwenye miaka 37, amekubali ofa ya kuwanoa Arsenal baada ya mazungumzo marefu ya saa 48. Atateuliwa rasmi baada ya mchezo wa City ugani Oxford.
Arteta alikuwa nahodha wa Arsenal na sasa ni chaguo bora kuwanoa. Amekubali kuwa kocha mpya wa Arsenal huku klabu hiyo kikiwa na matumaini kuwa atachukua ushukani wakati wa ziara yao ya Jumamosi, Desemba 21 ya kuelekea Everton.
Arteta atajaza nafasi ya Unai Emery ambaye alitimuliwa kwa kuandikisha matokeo mabovu katika mechi ya Ligi Kuu msimu huu.
Guardiola, kocha wa Manchester City, hata hivyo, anashikilia kuwa hana mpango wowote wa kuondoka klabu hiyo msimu ujao huku City ikihusishwa na kumteua kocha wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino kumrithi.
Awali, Arteta aliahidiwa na City mwaka jana kuwa atateuliwa kuwa mrithi wa Guardiola wakati ataondoka lakini sasa yaonekana hayo yatasalia kuwa ndoto.