This archive report was first published on 17 December 2019.
Rais Uhuru Kenyatta alizindua rasmi Bandari Kavu ya Kontena mjini Naivasha itakayopokea shehena kutoka Mombasa kutumia Reli ya Kisasa SGR.
Reli hiyo ina leni nne za kusafirishia abiria kutoka vituo vya; Ongata Rongai, Ngong, Mai Mahiu na Suswa na kituo kimoja cha kubadilishia leni kilichopo eneo la Nachu.
Bandari hiyo kavu (ICD) ipo kwenye reli mpya ya Nairobi-Suswa ambayo iliigharimu serikali KSh 150 bilioni.
Reli hiyo inatarajiwa kuboresha maendeleo katika eneo la Afrika Mashariki ikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda, Sudan Kusini na maeneo ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).
Alisema kazi ya kuboresha na kuanzisha huduma za reli ya zamani eneo la 2B kwenda Malaba inaendelea.
“Huduma ya kusafirisha kwenda Naivasha itasaidia sana katika kuondoa msongamano Nairobi na Mombasa na pia kurahisisha usafirishaji wa cargo kwenda maeneo ya Magharibi mwa nchi. Pia itasaidia Sudan Kusini, Rwanda, DRC na Uganda kupunguza muda wa kusafirisha shehena kutoka Bandari ya Mombasa,” alisema Rais Uhuru Kenyatta.