This archive report was first published on 17 December 2019.
Afya Yako: Fahamu kuhusu vidonda vya tumbo na kinachovisababisha ¶
Ukiongea kuhusu afya ya mwili wa binadamu, mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka chakula kufikia hali inayoweza kuvutwa na kuingia kwenye damu.
Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huu ni kinywa, umio, mfuko wa tumbo, ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba, kongosho, utumbo mpana na puru.
Hasa, kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula. Hii inatambulika kama 'Peptic ulcers'.
Watu wenye umri mkubwa ambao hutumia mara kwa mara dawa za kutuliza maumivu, kama vile aspirin na dawa zingine za kutuliza maumivu, zinazojulikana kama 'nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs)', zinaweza kuchochea kuta za tumbo na utumbo mdogo kufura.
Uvutaji wa sigara na matumizi ya pombe pia huongeza hatari ya kupata vidonda vya tumbo. Msongo wa mawazo pia husababisha vidonda moja kwa moja, lakini hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wenye vidonda hivyo.
Uvutaji wa sigara, matumizi ya pombe, na msongo wa mawazo ni kichocheo kikuu cha vidonda vya tumbo. Pia inadaiwa chembe za urithi 'Genetics' zinaweza kumfanya mtu kuwa na vidonda vya tumbo.