Skip to main content

Bungoma: Kaka amuharibia nduguye kazi kudai ni mwizi sugu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 17 December 2019.

Kituo cha Cheptais, Bungoma, kilikuwa na tukio la kusisimua baada ya kakake kudai alikuwa mwizi sugu. Hii ilikuwa baada ya ndugu yake kufaulu mahojiano ya kuwa karani katika kiwanda kimoja eneo hilo.

Alipokuwa amefaulu mahojiano, jamaa alipewa kazi, lakini ilikuwa vigumu kwake kuanza kazi kwani nduguye wa toka nitoke alianza kueneza fununu kwamba kalameni alikuwa na tabia ya kuiba.

Alipojaribu kufuatilia ili ajue kilichotokea, aliarifiwa ni kakake ambaye anahudumu katika kampuni hiyo alimchongea baada ya kumuonya meneja dhidi ya kumuajiri.

"Msikubali aanze kazi. Ana tabia ya kuiba vitu kila mahali anapopewa kazi," nduguye jamaa alimwarifu meneja.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →