Skip to main content

Wakili Ahmednasir Abdullahi atamwakilisha King Kaka mahakamani kwa ukiukaji wa jina

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 17 December 2019.

Wakili wa masuala ya kikatiba Ahmednasir Abdullahi amesema atamwakilisha King Kaka mahakamani kwa ukiukaji wa jina baada ya Gavana Waiguru kutishia kumshtaki kwa kumchafulia jina.

Abdullahi alisema hii kupitia ujumbe wake wa Twitter siku ya Jumanne, Desemba 17, 2019, baada ya Gavana Waiguru kutishia kumshtaki King Kaka kwa kumchafulia jina kupitia wimbo wake wa Wajinga Nyinyi.

Wimbo huo ulipakiwa YouTube siku ya Jumamosi, Desemba 14, 2019, na kukambutiwa vyema na Wakenya wengi.

King Kaka alikuwa anakashifu visa vya ufisadi ambavyo vimekithiri nchini kupitia wimbo huo.

Abdullahi alisema atamwakilisha King Kaka kwa sababu anahisi kwamba hakuna kiongozi yeyote aliyechafuliwa jina kupitia wimbo huo.

Alisema hii kupitia ujumbe wake wa Twitter: "Nilisema na nitarudia tena... nitatoa huduma za kisheria kwa King Kaka dhidi ya yeyote ambaye atamshtaki kwa wimbo wake wa Wajinga Nyinyi. Ninahisi kuwa hakuna mtu yeyote uongozini ama umma aliaribiwa jina."

Abdullahi alisema atamwakilisha King Kaka mahakamani kwa ukiukaji wa jina baada ya Gavana Waiguru kutishia kumshtaki kwa kumchafulia jina.

Wimbo huo ulikuwa unaashiria kuwa Gavana Waiguru alitumia KSh 8,000 kununua kalamu ya kuandikia kinyume na bei ya kawaida ya KSh 20.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →