This archive report was first published on 17 December 2019.
Gavana Waiguru atishia kumshtaki King Kaka kwa kumchafulia jina ¶
King Kaka alipakia wimbo huo kwenye Youtube siku ya Jumamosi, Desemba 14, ambapo alikuwa anakishifu visa vya ufisadi kupitia wimbo huo.
Waiguru pia anataka King Kaka kumuomba msamaha kwa kumhusisha na sakata ya wizi wa mamilioni ya fedha katika Shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS), kupitia wimbo huo.
Waiguru amezua kuwa wimbo huo umemchafulia jina kwa kumuita mtu fisadi, na ametoa makataa ya saa 48 kwa King Kaka kumuomba msamaha.
“Kwa niaba ya mteja wetu, tunakuagiza kuomba msamaha na kuondoa video hiyo mtandani katika kipindi cha saa 48 tangu kupokea barua hii,” ilisoma barua hiyo kutoka kwa wakili wa Waguru.
Waiguru anasema King Kaka anataka kujipatia umaarufu kwa kutumia jina lake, na wimbo huo umemfanya kuonekana kama kiongozi ambaye ni fisadi na alihusika katika wizi wa fedha za NYS.
Msanii King Kaka alikuwa anakishifu visa vya ufisadi kupitia wimbo huo, lakini Waiguru anasema wimbo huo umemsababishia hasara kubwa kwani msanii huyo analenga kutumia jina lake kujitafutia umaarufu.