This archive report was first published on 16 December 2019.
Khaligraph Jones: DJ Huyo Alimkera Kwa Kumtumia Sauti Za Kuudhi ¶
Desemba 12, 2019, jijini Nairobi, Chuo Kikuu cha Nairobi, siku ya Ijumaa, rapa maarufu Khaligraph Jones alikuwa akitumbuiza mashabiki wake katika hafla moja.
Alipokuwa akiimba wimbo wake wa Omollo, DJ huyo alimkera kwa kumtumia sauti za kuudhi, na kumpoteza kila mara.
‘Wakati uko kwenye jukwaa unatumbuiza watu na DJ anaanza kukwaruza huku akiweka jina lake kila mara baada ya sekunde tano na kuchezesha hizo sauti za kuudhi ambazo hukupoteza wakati unaimba, Buda acha ujinga, the OG aheshimiwe #respecttheogs,’ alisikia Khaligraph akimwambia DJ.
Alipomkera, Khaligraph alijitokeza kuelezea kisa hicho kwa kusema alikerwa na DJ huyo wakati alikuwa akiimba wimbo wake wa Omollo.
‘Nitakuchapa wewe, unafanya nini wewe. DJ ngoja hapo kwanza, buda sitaki mchezo hapa wewe. Ebu anzisha hiyo ngoma tena na ukiharibu tena tunakuchapa sai vibaya sana,’ alisikia Khaligraph akimwambia DJ.
Video hiyo iliyoibuka mtandaoni inaonyesha Khaligraph anaonekana akiimba wimbo wake kabla ya kusita ghafla na kuanza kumuendea DJ huyo kwa ubishi.
Alipomkera, mashabiki wake pia walisikika wakimshangilia wakati alipomuagiza DJ kumwachia mtu mwingine majukumu hayo.