This archive report was first published on 15 December 2019.
Gavana Mike Sonko ametakiwa kufika mbele ya mahakama ya Voi Disemba 18 kujibu mashtaka ya kumshambulia afisa wa polisi.
Agizo la Sonko kufika mahakamani lilitolewa na Kiongozi wa Mashtaka ya Umma Norrdin Haji baada ya kupekua faili ya mashataka iliyotumwa kutoka kituo cha polisi cha Voi.
Wakati wa kukamatwa, Sonko alitoa matusi na fujo alipokuwa akikataa kutiwa mbaroni na kuwazuia maafisa wa polisi kutekeleza kazi yao kisheria.
Alidaiwa kumshambulia mshirikishi wa eneo la Pwani Rashid Yakub wakati wa kukamatwa kwake katika uwanja mdogo wa ndege wa Voi.
Alidaiwa pia kumjeruhi afisa wa polisi aliyekuwa akiongoza kikosi cha polisi na kuharibu vifaa vya wanahabari.
Agizo la Sonko kufika mahakamani lilitolewa baada ya kupekua faili ya mashataka iliyotumwa kutoka kituo cha polisi cha Voi.