This archive report was first published on 14 December 2019.
Bungoma: Gavana Wangamati Aidhinisha U Nywaji wa Busaa Krismasi Hii ¶
Gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati ameamrisha wakazi wa kaunti hiyo kunywa pombe ya busaa msimu huu wa sherehe.
Alisema hali ngumu ya kiuchumi imewafanya watu kutokunywa vinywaji wapendavyo na kwamba pombe hiyo ya kienyeji ndio matumaini yao sasa.
Wangamati alisema kuwa, "Bwana kamishna, waache watu wetu wafurahie Krismasi kimtindo. Tusisikie eti vijana wako wamekamata mtu yeyote aliyepatikana akishereekea kuzaiwa kwa Yesu Kristu akinywa busaa kwa kuwa hiki ndio kinywaji cha pekee kinachopatikana rahisi," alisema.
Aliyekuwa gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka ambaye ni Spika wa Seneti aliweka saini katika sheria kuhusu vileo ya 2015.
Wangamati vilevile alimshauri kamishna wa kaunti hiyo Hassan Abdi dhidi ya kuwakamata watakaopatikana wakinywa busaa msimu huu wa sherehe.
Aliisema, "Ikiwa utawakamata watakaopatikana wakinywa busaa, basi utaanza na mimi," alisema.
Wakenya mitandaoni hasa kutoka eneo hilo wameupokea ujumbe wa Wangamati kwa mikono miwili.