This archive report was first published on 13 December 2019.
Maporomoko yameathiri barabara eneo la Chugor, Marakwet Mashariki, na KeNHA imewashauri madereva kuchukua tahadhari kubwa wanapokaribia eneo hilo.
Maporomoko hayo yameifunga sehemu ya barabara ya Kitale – Kachibora – Kapchero – Makutano – Kapyego – Chesoi – Chesongoch – Tot (B15) eneo la Chesoi.
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano wa KeNHA Charles Njogu alisema kwa sasa shughuli za magari eneo hilo zimetatizwa.
“Madereva wanashauriwa kuchukua tahadhari kubwa wanapokaribia eneo hilo na kufuata maelekezo ya polisi trafiki na maafisa wetu eneo hilo,” Njogu alisema.
Aliwashauri madereva kutumia barabara ya Biretwo – Tot.
KeNHA imewasiliana na mkandarasi kuondoa vifusi sehemu hiyo ya barabara ili kuregesha usafiri kawaida.
Maporomoko hayo yameathiri barabara kwa sababu ya mvua ambazo zimekuwa zikinyesha maeneo mengi ya humu nchini na hata kusababisha maafa Pokot Magharibi, na watu kuhama makazi yao kwa mafuriko.