Skip to main content

Wakenya wamsuta Rais Kenyatta kwa kutaka wabunge wasiwe mawakili

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 13 December 2019.

Wakenya wamsuta Rais Kenyatta kwa kutaka wabunge wasiwe mawakili

Wakenya wamesema Rais Uhuru Kenyatta hawezi kuwakosoa viongozi waliochaguliwa ambao wanafanya kazi pia kama mawakili.

Aliongea wakati wa sherehe za Jamhuri, Disemba 12, katika uwanja wa Nyayo, Rais Uhuru Kenyatta alisema wabunge au maseneta kuhudumu kama mawakili ni kula kuwili.

"Mwalimu hawezi akawa na mguu mmoja darasani na mwingine mbungeni, huwezi ukahudumu kama mbunge na bado ushikilie taaluma ya kisheria," Uhuru alisema.

Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa muungano wa NASA Norman Magaya alimkumbusha Rais kuwa aliwahi kupokea huduma za mawakili ambao walikuwa ni wabunge wakati huo.

"Marehemu Mutula na Orengo walimwakilisha Uhuru wakati walikuwa wabunge," Magaya alisema.

Magaya alimtaka Rais Kenyatta kushughulikia matatizo mengine ambayo yanaikumba nchi badala ya kuangazia nguvu zake kwa masuala kama ya washukiwa wa ufisadi kuwakilishwa na viongozi waliochaguliwa.

Aliyekuwa mwanaharakati David Ndii alisema Rais Uhuru Kenyatta hawezi kuwakosoa viongozi waliochaguliwa ambao wanafanya kazi pia kama mawakili.

"Uhuru Kenyatta kuongea kuhusu watu kujinufaisha kuwili ni kama yule mbunge alienda mkutano kuhusu kukabiliana na pombe haramu akiwa mlevi," Ndii alisema.

Wakenya wamesema Rais Uhuru Kenyatta hawezi kuwakosoa viongozi waliochaguliwa ambao wanafanya kazi pia kama mawakili. Picha: State House

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →