This archive report was first published on 13 December 2019.
Seneta wa Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen, na mkewe Gladys Wanjiru wanasherehea miaka 10 ya ndoa.
Alhamisi, Disemba 12, 2019, Murkomen aliadhimisha miaka 10 ya ndoa kwa kushiriki picha ya harusi yao iliyofanyika mwaka wa 2009 kwenye Instagram.
Aliimba pia kwa Mungu kwa kuibariki na kuifanikisha ndoa yake.
"Miaka 10 katika ndoa, asante Mungu," Murkomen aliandika Instagram.
Mashabiki wao mitandaoni bila kusita waliwatakia wanandoa hao maisha marefu na ndoa ya kudumu.