This archive report was first published on 13 December 2019.
Video inayosambaa mitandaoni inaonyesha mchuuzi mmoja akiyaosha matunda akitumia maji taka ya mtaroni kabla ya kuyapeleka sokoni.
Ingawa TUKO.co.ke haiwezi kuthibitisha ni lini video hiyo ilichukuliwa, mchuuzi huyo alikuwa akiyaosha matunda hayo kwa nia ya kuyauza barabarani, labda kwa watu wasiokuwa na ufahamu yalivyopakiwa.
Wakenya wameshangazwa sana na video hii, ambayo inaonyesha kuwa baadhi ya wachuuzi wanaosha matunda barabarani hawana ufahamu wa hatari zinazoweza kutokea.
Ingawa watu wengi hununua matunda yanayouzwa na wachuuzi barabarani na kuyala hususan wanapokuwa safarini, kwa video hii itawabidi kuwa makini mno.
Matunda ni mojawapo ya viungo muhimu vya lishe bora, lakini yanaweza yakasababisha maradhi hatari mwili ikiwa yataliwa kabla ya kuyaosha.
Wakenya wamejiuliza maswali mengi na wengine hata kugundua kwamba wamewahi kuyanunua matunda na kuyala bila ya kuyaosha kwa maji safi barabarani.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.