This archive report was first published on 10 December 2019.
Uchaguzi wa 2022 unakuja kwa haraka, na Abduba Dida, aliyekuwa mgombea wa urais, amesema kuwa Wakenya watakuwa na maisha magumu ikiwa Naibu Rais William Ruto atachaguliwa kuwa rais mwaka wa 2022.
Amesema hili kwa kutumia ukurasa wake wa Twitter, na kuongeza kuwa huenda asilimia kubwa ya Wakenya wakahama humu nchini kwa ajili ya uchumi mbovu na maisha kuwa ghali.
Amesema, "Iwapo Jubilee itashinda uchaguzi mkuu 2022 chini ya uongozi wa William Ruto, basi Wakenya wengi watahama nchini. Maisha yatakuwa magumu kupindukia, tumebakisha miaka mitatu tu kubaini ukweli," Dida aliandika Twitter.
Amesema hili wakati Ruto ametangaza azma ya kumrithi Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu 2022.