Skip to main content

Afya Yako: Vyakula 7 vyenye afya vitakavyokusaidia kupambana na baridi

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 10 December 2019.

Afya Yako: Vyakula 7 vyenye afya vitakavyokusaidia kupambana na baridi

Katika kipindi cha mvua nyingi, hali ya baridi inashuhudia maeneo mengi ya nchini. Mwili hutakiwa kuwa na joto linalohitajika, la sivyo huenda mwili ukakumbwa na magonjwa yasababishwayo na baridi na muda wako mrefu ukapotezea kitandani.

Wakati huu, vyakula fulani vinaweza kutoa joto na nguvu kwa mwili. Kwa mfano, chai iliyotiwa tangawizi ina manufaa ya afya kwa sababu ina virutubisho vya ginger ambavyo vinaweza kutoa joto na kuimarisha mfumo wa kinga wa mwili.

Utafiti uliofanywa katika chuo kimoja jijini London ulionyesha kuwa, mtu anayekunywa kahawa huwa na uelewa zaidi ikilinganishwa na asiekunywa. Magonjwa kama vile saratani, kisukari, matatizo ya maini na vilevile akili yameonekana kuwapata watu wasiokunywa kahawa.

Shayiri ina virutubisho muhimu zaidi (nyuzi) visivyopatikana katika nafaka zingine na ina uwezo wa kupunguza Cholesterol mwilini. Ndizi zina virutubisho vya aina mbalimbali kama vile, protini, mafuta, kalishiamu, wanga, fosiforas, madini ya chuma, vitamin A, B, C na maji.

Malenge yana Vitamini A, E, na C, na pia kiasi kikubwa cha potasiamu, kalsiamu, magnesiamu, iodini, cobalt, fluorine, klorini. Nyama nyekundu ni muhimu kwa afya ya binadamu, lakini itakuwa muhimu zaidi kama itatumiwa kwa kiwango na kiasi kinachotakiwa.

Viazi vitamu vina faida nyingi sana mwilini, ikiwa ni pamoja na kutoa usingizi mzuri na kuboresha afya ya macho. Pia, malenge yana virutubisho muhimu kwa afya ya mwili, ikiwa ni pamoja na potasiamu, kalsiamu, magnesiamu, iodini, cobalt, fluorine, klorini.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →