This archive report was first published on 9 December 2019.
Mara baada ya kuingia kitandani siku ya Jumapili, Disemba 8, Mama Baha alianza kuhisi maumivu tumboni mwake. Alitangaza habari hizi mwenyewe kupitia kwenye mtandao wa Instagram.
Alipofika hospitalini, madaktari wamesema yuko katika hali mbaya, lakini Mama Baha anaamini atapata afueni ya haraka.
Alipotangaza habari hizi, mashabiki wamemtakia afueni ya haraka.
Alisema, "Leo ilikuwa siku kama nyingine ile, nilienda kuogelea kisha nikarejea nyumbani, baada ya kuvalia nguo zangu za kulala, nilihisi maumivu tumboni, nilienda hospitali na daktari akaniambia niko katika hali mbaya, hata hivyo naamini ripoti ya Mola zaidi, najua nitapona haraka," Mama Baha aliandika Instagram.