This archive report was first published on 9 December 2019.
Mwanawe wa kiume wa aliyekuwa naibu wa rais Kijana Wamalwa ameaga dunia akiwa nyumbani kwao mtaani Milimani mjini Kitale.
Aliaga dunia Jumapili, Disemba 8, 2019, kutokana na ugonjwa wa kisukari, kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa familia yake.
Robert Wamalwa, baba wa marehemu, alisema, "Mpwa wangu alikuwa akiugua kutokana na ugonjwa wa kisukari, huenda huo ndio uliosababisha kifo chake, hata hivyo tunasubiri mwili wake ufanyiwe upasuaji ndiposa tubaini kilichomuua," kwa mujibu wa Daily Nation.
Wamalwa alitupilia mbali madai kuwa marehemu alifariki kutokana na unywaji pombe kupita kiasi na kwamba pia alikuwa akisumbuliwa kimawazo.