Skip to main content

Mkasa wa Tassia: Idadi ya Waliofariki Yaongezeka hadi Watu 10

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 9 December 2019.

Shughuli ya uokoaji inaendeshwa na wanajeshi wa KDF, Idara ya Kitaifa ya Kukabiliana na Majanga na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Watu 36 wameweza kuokolewa lakini watu saba bado hawajulikani waliko.

Operesheni hiyo inaendeshwa pole pole kwani waokoaji wanaamini kuwa bado kuna watu zaidi ambao wamekwama kwenye vifusi ni wangali hai na hivyo uchimbaji wafanywa kwa njia ya utaratibu.

Matumaini ya Kamishna msaidizi wa Embakasi James Wanyoike ni kwamba zoezi hilo litakamilishwa siku ya Jumatatu, Desemba 9.

"Kwa bahati, endapo hatutasumbuliwa na mvua, kufikia leo jioni huenda tutakuwa tumemaliza. Lazima tusafishe eneo la tukio. Hatuwezi kuwacha vifusi," alisema Wanyoike.

Shughuli ya uokoaji inaendeshwa kwa njia ya utaratibu ili kuzuia kuwajeruhi waliokwama na bado wangali hai.

Watu saba hawajulikani waliko huku familia zao zikiendelea kukita kambi katika eneo la tukio kusubiri kutangamana nao.

Matukio hayo yalichukua eneo la Tassia, Embakasi, Nairobi.

Idadi ya waliofariki iliongezeka hadi watu 10 baada ya miili tatu, mbili ya watoto na mwanamume, kuongezwa siku ya Jumapili.

Watu wawili wa kiume, miaka 11 na sita, waliondoka nyumbani saa mbili asubuhi na kuniambai walikuwa wanaenda kumtembelea jamaa yetu katika jumba hilo lililoporomoka.

"Hata hivyo, niliamushwa na kamsa. Nilipokimbia nje, niliambiwa eti jengo la orofa sita limeporomoka...Nawataka tu wapatikane wakiwa hai hata kama watakuwa na majeraha," alisema Gachomba akiwa na machozi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →