Skip to main content

Kocha Pep Guardiola akiri ni vigumu kumkimbiza Rashford kwani ana guu la almasi ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 8 December 2019.

Kocha Pep Guardiola akiri ni vigumu kumkimbiza Rashford

Debi ya Manchester iliyosakatwa siku ya Jumamosi, Desemba 7, 2019, ilikuwa mchezo muhimu kwa Manchester City na Man United.

City walipata matokeo mabovu wakati wa kushindwa kwa 2-1, huku Rashford na Martial wakionja wavu kila mmoja.

Guardiola alikiri kuwa masogora wake walishindwa maarifa na wageni wao, akiwemo Daniel James.

"Tulipoteza sana nafasi sio kawaida lakini zaidi ya mwaka jana dhidi ya United," alisema Guardiola.

"Tunajua kufyatuka kwao, huku James, Martial na Rashford, lakini wakati mwingine sio rahisi kuwazuia," aliongeza.

Ushinde huo uliwaacha wenyeji wa Etihad wakishikilia nafasi ya tatu na pointi 32 na 14 nyuma ya viongozi Liverpool.

United, kwa upande wao walijipunguzia presha na kuwa katika nafasi nzuri baada ya ushindi huo na kupanda hadi nafasi ya tano kwenye jedwali.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →