This archive report was first published on 8 December 2019.
Mhubiri Victor Muteru awavunja mbavu wanamtandao na 'injiri ya bwana' ¶
Victor Muteru, mtoto wa miaka 9, amevunja mbavu wanamtandao na 'injiri ya bwana' baada ya kutoa ushuhuda wake kwenye runinga ya KDTV.
Ushuhuda wake ulikuwa wa kujieleza kwa namna ambayo wengi huwacha wakijiuliza kama kweli ni mtoto au mtu mzima aliye na mwili wa mtoto.
Alisema, "Kile ambacho ni muhimu kwangu mimi ni kuwa nina nguo za kuvaa, chakula na afya nzuri," na kuonyesha kuwa amekuwa mtu wa kutosheka na yale Mungu amempa na hivyo kuishi maisha matamu.
Video ya Victor ilikuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa wengi wamekuwa tu wakimwaga machozi ya kicheko.
Wanamtandao walikosa kuamini macho yao baada ya kutazama video ndogo ya Victor baada ya mahojiano na runinga ya KDTV.
Alipokatiza ushuhuda wake na kuanza wimbo kama jinsi ambavyo wahubiri waliobobea hufanya, baadhi ya wanamtandao walisema pasta Victor si mtoto ila mtu mzima na hata kuitaka serikali kuanza kuokota ushuru kutoka kwake.