This archive report was first published on 8 December 2019.
Viongozi wa Bonde la Ufa Wanataka Refarenda Ifanyike Agosti 2021 ¶
Wakiongozwa na aliyekuwa gavana wa Bomet Isaac Ruto na mbunge wa Cherang'any Joshua Kutuny, viongozi hao walisema kamati inafaa kuundwa ili iokote sahihi za kuanzisha mchakato wa refarenda.
Walisema bunge linafaa kuharakisha na kuunda sheria kuhusu refarenda sawa na kufanyia tume huru ya mipaka na uchaguzi (IEBC) mageuzi ili iwe tayari kuendesha kura ya maamuzi.
Wananchi wanafaa kuachiwa nafasi ya kuamua kuhusu BBI, na serikali inapaswa kushughulikia hali ya kiuchumi nchini kwa sasa wakiteta kuna uhaba wa fedha.
Alama ya kundi hilo ni sawa na ule wa viongozi wengine pia kutoka bonde la ufa wanaoegemea upande wa Naibu Rais William Ruto.
Published on December 8, 2019