Skip to main content

Mshukiwa wa Mauaji Peter Mugure Atasalia Korokoroni Kwa Siku 12

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 7 December 2019.

Aliyekuwa mwanajeshi Peter Mugure anashukiwa kuwatoa uhai wanawe wawili pamoja na mpenziwe. Picha: Citizen

Atasubiri siku 12 kabla ya kujibu mashtaka hayo.

Ukaguzi wa kiakili ulikuwa umefanyika katika hospitali ya rufaa ya Nanyuki, lakini daktari aliyekuwa amemfanyia ukaguzi huo alikataa kutia sahihi fomu ya shughuli hiyo.

Wakili wa serikali Peter Mailanyi alisema mahakama kwamba ukaguzi huo ulikuwa umefanyika katika hospitali ya rufaa ya Nanyuki na daktari huyo.

Ataendelea kuzuiliwa katika jela la King'ong'o akisubiri kufanyiwa ukaguzi wa kiakili ili ajibu mashtaka ya mauaji hayo.

Wakili wa serikali aliambia mahakama kuwa usalama wa mshukiwa uko hatarini iwapo kesi itaendelea kuskizwa katika mahakama ya Nanyuki.

Wananchi waliokuwa na hamaki walipiga kambi nje ya mahakama hiyo wakitaka kumpa funzo mshukiwa huyo.

“Wananchi walijaa mahakamani na walitaka kumshambulia na tulilazimika kumlinda. Ripoti za ujasusi zinasema usalama wa mshukiwa upo hatarini,” wakili wa serikali alisema.

Hiyo ilifanya kesi hiyo kuhamishwa kutoka mahakama hiyo ya Nanyuki mpaka korti ya Nyeri.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →