This archive report was first published on 6 December 2019.
Mzee kutoka eneo la Muutine, jimbo la Meru, alikuwa na shida ya kibinafsi ambayo ilimfanya ajiandaa kwa kiasi kikubwa.
Alilazimika kusaka maombi kutoka kwa pasta ili amnasue mkewe kutokana na pepo la ulevi.
Wawili hao walikuwa wameishi katika ndoa kwa miaka kumi na walikuwa washirika wa kutegemewa sana kanisani.
Aligundua kuwa mienendo ya mama yake imebadilika kwani alianza kususia ibada za kanisani.
Uchunguzi wa mzee ulibaini kwamba alikuwa akinyemelea kwa mama pima kisiri kukata kiu cha dozi.
Aliamua kubisha hodi kwa pasta ili amuombee mkewe abadili mienendo kwa kuwa alihisi huenda amerogwa.
Pasta alifika bomani kwa wawili hao, lakini hawakumkuta mama, lakini baada ya muda mfupi aliwasili akiwa amelewa chakari na kupata maombi yanaendelea.
Mama alianza kuropokwa na kumkemea pasta akisema yeye hakuhitaji maombi ya mtu yeyote.
"Hakuna haja ya kunifanyia dua kwani hamna aliye msafi. Mimi nitapambana na hali yangu msiwe na wasiwasi," mama alisema.